Maswali

Unachohitaji kujua kuhusu Hifadhi Biashara

1. Hifadhi Biashara ni nini?

Hifadhi Biashara ni bima ndogo iliyoundwa kwa ajili ya kulinda wenye biashara ndogo na familia zao.

2. Nani anaweza kununua Hifadhi Biashara?

Mtu yoyote mwenye biashara ndogo.

3. Nawezaje kununua Hifadhi Biashara?

Unaweza kununua Hifadhi Biashara katika simu yako ya mkononi kwa kutumia Selcom kupitia app ya Duka Direct au TigoPesa au kupiga namba ya USSD *150*01 #. Bonyeza hapa kupata mwongozo wa jinsi ya kununua bima.

4. Hifadhi Biashara inafidia nini?

Uharibifu wa mali: Kwa madai dhidi ya moto, mlipuko, mafuriko, tetemeko la ardhi, matendo ya Mungu, ghasia na mgomo nk.
Wizi: Ikiwa bidhaa zako zimeibwa katika eneo lako la kazi.
Kodi: Kwa gharama ya kodi hadi siku 10 kufuatia madai ya uharibifu wa mali.
Upotevu wa Pesa: Kwa pesa zilizoibiwa katika eneo lako la kazi au zilizoporwa.
Gharama ya mazishi: Katika tukio la kifo tutafidia gharama za mazishi.

5. Fidia zina kiwango gani?

Uharibifu wa mali: Tunafidia hadi TZS 5,000,000
Wizi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000
Kodi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000
Upotevu wa pesa: Tunafidia hadi TZS 250,000
Gharama za mazishi: Tunafidia hadi TZS 1,000,000

6. Hifadhi Biashara inagharimu kiasi gani na unalipaje?

Malipo ya mwaka ni TZS 84,000, ingawa unaweza kulipa TZS 7000 kwa mwezi, TZS 21,000 kwa miezi mitatu na TZS 42,000 kwa miezi sita au TZS 84,000 mara moja kwa mwaka.

7. Bima inakulinda kwa muda gani?

Hifadhi Biashara inakulinda kwa wakati wote uliolipia bima yako. Malipo ya mwaka ni TZS 84,000, ingawa unaweza kulipa TZS 7000 kwa mwezi, TZS 21,000 kwa miezi mitatu na TZS 42,000 kwa miezi sita au TZS 84,000 mara moja kwa mwaka.

8. Ninaweza kupata bima yenye mpango wa malipo kubwa zaidi ikiwa biashara yangu sio ndogo?

Unaweza kupata/kuchagua bima iliyo kubwa zaidi. Tutathamini biashara yako na kukupa taarifa zaidi. Wasiliana nasi kwa njia yay barua pepe kupitia info@howdenpuri.co.tz

9. Naweza kujiondoa katika bima/huduma ya Hifadhi Biashara?

Ndio, kwa kusitisha malipo yako, unatolewa katika bima ya Hifadhi Biashara moja kwa moja.

10. Nawezaje kudai fidia?

Unaweza kudai fidia kupitia app ya Duka Direct, app ya TigoPesa au kupiga USSD *150*01#. na kufuata maelekezo. Madai yote yatakayokidhi vigezo yatafidiwa ndani ya muda wa masaa 72/siku 3. Endapo habari zaidi zitahitajika kuhusu madai yako tutawasiliana nawe. Kwa maelezo zaidi bofya hapa. Kwa madai ambapo ushahidi wa picha unahitajika (uharibifu wa mali na mazishi), italazimika kutuma picha zako kupitia linki hii