Fidia ya kodi

Kama umepata hasara kutokana na uharibifu wa mali, unaweza kuwa na matumizi mengine kama kulipa kodi. Ndani ya siku kumi baada ya tukio, tutafidia hadi TZS 1,000,000 kama huwezi kuendesha biashara yako kwa sababu ya uharibifu wa mali.

Unachohitaji kufanya ni kutujulisha kwa simu yako na kufuata maelekezo mepesi. Aidha utatuma nakala ya mkataba wa kodi ya pango na kiasi unachohitaji tufidie.

Kama kila kitu kiko sawa, tutafidia hasara yako ndani ya siku 3 kwenye simu yako.

Kwa taarifa zaidi soma hati ya bima kwa Kiswahili au Lugha ya Kingereza au wasiliana na Sanlam au Howden Puri