Uharibifu wa mali

Eneo lako la biashara na mali/vifaa vyako vya biashara kwa ujumla vinaweza kuharibiwa na matukio nje ya uwezo wako kama moto, maji, milipuko au majanga asilia kama matetemeko, mafuriko au maporomoko ya ardhi.

Kama umepatwa na tatizo la namna hii, tutafidia hasara yako hadi TZS 5,000,000 ndani ya mwaka mmoja.

Unachohitaji kufanya ni kutujulisha kwa simu yako na kufuata maelekezo mepesi. Aidha utatuma picha zinazoonyesha mali/vifaa vyako vilivyoharibika, ushaidi wa kuwa mwenye mali pamoja na kiasi cha kufidia.

Kama kila kitu kiko sawa, tutafidia hasara yako ndani ya siku 3 kwenye simu yako.

Kwa taarifa zaidi soma hati ya bima kwa Kiswahili au Lugha ya Kingereza au wasiliana na Sanlam au Howden Puri